- 3,812 viewsDuration: 3:11Familia mbili katika kaunti ya Mombasa zinalilia haki baada ya wapendwa wao kuuwawa katika hali tatanishi. Katika kisa cha kwanza, Elizabeth Nina aliuwawa na mwili wake kutupwa katika nyumba iliokuwa ikijengwa huko Likoni. Familia yake inadai aliwaarifu kuwa alikuwa anaelekea kwa rafikiye kabla ya kutoweka. Katika kisa kingine, familia ya Gloria Kaiza, mwanafunzi wa gredi ya 5 aliyedaiwa kubakwa na kisha kuuwawa huko kisauni inalalamikia kujikokota kwa uchunguzi na kukamatwa kwa mhusika.