- 7,550 viewsDuration: 1:53Mwili wa mwanamke uliokuwa ukizozaniwa na wanaume wawili umeondolewa katika makafani ya Kilifi baada ya mahakama ya Mombasa kuagiza mumewe wa kwanza kuzika mwili Huo. Marehemu Saumu Luvuno aliaga dunia tarehe 7 machi na mwili wake kudaiwa kuibwa katika makafani makadara kabla ya familia kuelekea mahakamani. Familia imetaka waliotekeleza kitendo hicho kuchukuwa hatua kali. Wanadai baadhi ya maafisa katika makafani ya makadara walishirikiana kuhamisha mwili huo kinyume na agizo lao.