Skip to main content
Skip to main content

Familia sita zinalilia haki baada ya wanafunzi wa chuo cha Laikipia kupigwa risasi na polisi

  • | Citizen TV
    4,881 views
    Duration: 3:29
    Familia sita za wanafunzi wa Chuo cha Laikipia zinalilia haki baada ya watoto wao kupigwa risasi na polisi wakati wa maandamano siku ya Jumatatu. Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 19 alifariki wakati wa maandamano hayo huku wengine watano wakisalia hospitalini na majeraha ya risasi. Wanafunzi walikuwa wakiandamana kulalamikia kile walichodai ni utepetevu wa usimamizi wa chuo hicho kwa kukosa kufika haraka kumsaidia mwenzao aliyeanguka kwenye maporomoko yaliyotokea subukia siku ya Ijumaa.