- 2,592 viewsDuration: 2:42Familia tano katika kaunti ya Mombasa zinatafuta majibu kuhusu kutoweka kwa jamaa zao katika njia isiyoeleweka. Familia hizo zilizofika katika makao makuu ya polisi pwani zinawalaumu maafisa wa kitengo cha kupambana na ugaidi (ATPU), zikisema jamaa hao walichukuliwa na polisi. Na kama anavyoarifu Francis Mtalaki, baadhi ya waliotoweka wanadaiwa kufikishwa mahakamani kabla ya kutoweka kabisa.