- 5,217 viewsDuration: 3:02Chama tawala cha UDA kimepata pigo kubwa katika chaguzi ndogo za wadi kadhaa, huku chama cha Naibu Rais wa zamani Rigathi Gachagua kikivuna pakubwa. DCP ilijizolea viti vitatu vya uwakilishi wadi, ikiwemo maeneo yanayochukuliwa kuwa ngome za serikali. Ushindi katika Wadi ya Narok Mjini, Wadi ya Kisa, na Wadi ya Kariobangi North ukionekana kama kauli kali ya kisiasa kutoka kwa upinzani, na kuashiria ushindani mkali kisiasa katika Uchaguzi Mkuu wa 2027.