- 1,250 viewsAliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua amesema yuko tayari kupokea uamuzi wowote utakaotolewa kesho na majaji watatu wa Mahakama Kuu katika kesi ya kupinga kuondolewa kwake madarakani. Akizungumza baada ya kufanyiwa maombi maalum katika Kanisa la PCEA Muteero jijini Nairobi, Gachagua aliwataka wafuasi wake kudumisha utulivu na kuheshimu sheria bila kujali matokeo ya kesi hiyo. Kauli yake inajiri huku akisubiri kwa hamu uamuzi wa mahakama ambao unaweza kuwa na athari kubwa kwa mustakabali wake wa kisiasa.