- 8,640 viewsDuration: 1:25Miss Uganda alipotokea katika mashindano ya Miss World nchini Vietnam, gauni lake lilivutia hisia na kuzua mjadala kutokana na ujumbe uliobebwa na ubunifu wake. Gauni hilo lilibuniwa kuwakilisha tabaka saba za mwili zinazohusishwa na upasuaji wa kujifungua (C-section), huku kila tabaka likiwasilishwa kwa njia ya kisanaa. Kupitia kila mshono, mbunifu Mushirah Abdallah alitoa heshima kwa makovu ambayo akina mama wengi huyabeba kimya kimya, akigeuza simulizi ya upasuaji wa kujifungua kuwa kazi ya sanaa. #missuganda #bbcswahili #ugandatiktok Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw