Gavana Natembeya amehojiwa kutwa nzima na maafisa wa EACC

  • | Citizen TV
    5,691 views

    Vurugu zilishuhudiwa nyumbani kwa gavana wa trans nzoia, george natembeya, maafisa wa tume ya ufisadi eacc walipofanya msako wa ghafla uliodaiwa kuhusiana na matumizi mabaya ya shilingi bilioni 1.4 za kaunti. Msako huo wa alfajiri huko kitale uligeuka baada ya vijana waliokuwa na hasira, kupinga upekuzi huo na kuharibu magari manne ya eacc. Gavana natembeya alikamatwa baadaye na kupelekwa katika afisi za eacc jijini nairobi, ambako alirekodi taarifa kuhusu madai hayo.