Gavana wa kaunti ya Trans Nzoia, George Natembeya, ameitaka serikali ya kitaifa kushirikiana na serikali ya kaunti kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo kwa bei nafuu, hatua itakayosaidia kuimarisha sekta ya kilimo nchini.
Akizungumza katika wadi ya Hospital, wakati wa hafla ya kugawa zaidi ya wakulima 10,000 mbegu za bure, Natembeya amesema kwamba serikali yake imehakikisha zaidi ya wakazi 300,000 wanapokea mbegu bila malipo, licha ya changamoto za kiuchumi zinazowakabili wakulima, hususan kupata mbolea inayohitajika kutoka serikalini.
Viongozi pia wamesisitiza wanasiasa kuangazia masuala halisi yanayowakabili Wakenya, kama vile hali ngumu ya kiuchumi, ili kupunguza mzigo wa raia wa kawaida.