- 313 viewsDuration: 59sWakazi wa eneo bunge la Ol Kalou wametakiwa kudumisha amani wanapojiandaa kushiriki uchaguzi mdogo utakaofanyika Alhamisi wiki hii. Akizungumza huko Ol Kalou, gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru amesema siasa za fujo hazina nafasi katika jamii ya kidemokrasia. Amewataka viongozi wa kisiasa na wananchi kuhubiri amani, kuheshimu sheria, na kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa utulivu na uwazi.