Skip to main content
Skip to main content

Gereza la wanene

  • | BBC Swahili
    7,859 views
    Duration: 2:33
    Nchini China kuna kambi maalumu za kupunguza uzito ambazo baadhi ya watu wamezibatiza jina la “magereza ya watu wanene” kutokana na nidhamu kali na masharti yanayotumika. Washiriki hulazimika kufanya mazoezi kwa ratiba maalumu, kufuata mgao wa chakula na kupimwa uzito mara mbili kwa siku. Mtengeneza maudhui TL Huang, maarufu kama Eggeats, anasema alikaa kambini kwa siku 28 bila kuruhusiwa kutoka na hatimaye kufanikiwa kupunguza uzito. Hata hivyo, wataalamu wa lishe wanaonya kuhusu hatari za mbinu kali za kupunguza uzito na kusisitiza umuhimu wa kuzingatia afya na njia salama na endelevu. Mwandishi wa BBC @mariammjahid na maelezo zaidi. 🎥: @frankmavura Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw