- 1,811 viewsDuration: 3:43Gharama ya masomo ya chuo kikuu inaendelea kuwalemea wanafunzi wengi miaka mitatu baada ya mfumo mpya kuanza kutekelezwa. Hali hiyo imemsababisha mwanafunzi mmoja wa mwaka wa pili wa udaktari katika Chuo Kikuu cha Nairobi kugeukia kazi ya mjengo ili kumudu karo na kupata pesa za kujikimu chuoni. Kijana huyo hulazimika kukosa masomo mara kwa mara akitafuta kazi za sulubu. Si yeye pekee anayekabiliwa na hali ngumu chuoni. Mwanafunzi mwingine wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Kabianga yuko pia kwenye hatari ya kuacha masomo kutokana na gharama ya chuo kikuu.