Skip to main content
Skip to main content

Ghasia Nanyuki huku wakazi wakipinga kituo cha karantini ya Ebola

  • | Citizen TV
    809 views
    Ghasia na makabiliano yalishuhudiwa mjini Nanyuki leo baada ya mamia ya wakazi kuandamana wakipinga kuwepo kwa kituo cha karantini ya Ebola katika kambi ya Laikipia Airbase. Kituo hicho, kinachotarajiwa kuhudumia raia wa Marekani waliokumbwa na virusi vya Ebola, kimezua hisia kali miongoni mwa wananchi na kuibua mjadala kuhusu mamlaka ya Kenya pamoja na uwezo wa mfumo wake wa afya kukabiliana na magonjwa hatari. Waandamanaji walitaka uwazi zaidi kuhusu makubaliano yaliyopelekea kuanzishwa kwa kituo hicho na kueleza wasiwasi wao kuhusu usalama wa afya ya umma. Kama anavyoripoti Brenda Wanga, mtu mmoja alijeruhiwa wakati wa maandamano hayo.