- 204 viewsDuration: 2:46Serikali ya kaunti ya nairobi imeamuru wajenzi wa majengo ya ghorofa ndefu katika eneo la kileleshwa kugharamia ukarabati wa miundomsingi ya umma iliyoharibiwa, ikiwemo mifumo ya majitaka. Agizo hilo limetolewa kutokana na malalamishi kutoka ubalozi wa uholanzi, ambao unasema ujenzi wa jengo la ghorofa karibu na makazi yake umesababisha mafuriko . Wakazi wengine wa kileleshwa pia wamelalamika kwamba tatizo hilo limekithiri.