- 1,231 viewsDuration: 1:43Gitau Munene na Evans Kili wameibuka mabingwa wa mashindano ya Kaptagat 4x4, wakitwaa ushindi katika viwango vya wataalamu na wanaoanza mtawalia. Mashindano ya mwaka huu yalivutia zaidi ya washindani 20 waliokuwa wakishindania zaidi ya shilingi 180,000 pesa taslimu huku wakipata uzoefu muhimu kwa mashindano yajayo. Washiriki walielezea njia hiyo kuwa ya kiufundi na yenye changamoto kubwa, wakisema imewapa uzoefu muhimu wa kukabiliana na mashindano magumu zaidi katika mfululizo ujao baadaye mwaka huu.