Skip to main content
Skip to main content

Hasara ya mgomo wa wafanyakazi wa sekta ya usafiri wa anga Kenya

  • | BBC Swahili
    14,406 views
    Duration: 2:36
    Mgomo wa wafanyakazi wa sekta ya usafiri wa anga nchini Kenya umesitishwa baada ya zaidi ya saa 18 za mazungumzo. Serikali na wafanyakazi wamefikia makubaliano, huku wafanyakazi wakirejea kazini na juhudi za kurejesha huduma za kawaida zikianza. Mgomo huo wa siku mbili ulivuruga safari na kuwaacha maelfu ya wasafiri wamekwama, huku hasara ikikadiriwa kufikia dola milioni 5. Mwandishi wa BBC Laillah Mohammed ametuandalia taarifa hii. 🎥: @frankmavura #bbcswahili #kenyakaa #usafiriwaanga Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw