Skip to main content
Skip to main content

Hatimaye familia ya Jackson Tito imepewa makao

  • | Citizen TV
    1,439 views
    Ilikuwa furaha kwa Jackson Tito na familia yake baada ya kukabidhiwa nyumba mjini Machakos, kufuatia ahadi iliyotolewa na serikali. Tito, ambaye katika siku za hivi karibuni amejulikana na wengi kufuatia taarifa kuhusu majukumu alioachiwa ya kuwalea ndugu zake wanne, alisema maisha yao yamebadilika kwa kasi isiyotarajiwa. Mama yake alieleza kutokuamini alichokiona kwani sasa wametoka maisha ya uchochole hadi kuwa na makao bora. Familia ya Tito imekabidhiwa nyumba ya vyumba vitatu katika mradi wa nyuma za serikali mjini Machakos. Ndugu zake wamesajiliwa kujiunga na Shule ya Wavulana ya St. Mary’s mjini Machakos ambapo Mwalimu Mkuu Angelline Nzioki ameahidi kuwapa mazingira bora ya kusoma.