Skip to main content
Skip to main content

Hofu Kirinyaga: Wagonjwa wa figo waumia baada ya mashine kuwa mbovu kwa miezi 5

  • | Citizen TV
    1,149 views
    Duration: 2:52
    Wagonjwa wa Figo katika kaunti ya Kirinyaga wanahofia kukosa matibabu katika hospitali ya Kerugoya baada ya mashine za kusafisha figo kuharibika. Mashine hizo ambazo hutoa huduma kwa wagonjwa wote wa figo katika kaunti hiyo zimekuwa zikiharibika mara kwa mara katika muda wa miezi mitano iliyopita. Kwa sasa ni mashine mbili tu kati ya nane inayofanya kazi, hali ambayo imewaacha wagonjwa na mahangaiko chungu nzima.