- 29 viewsDuration: 3:25Huku mvua ikiendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali humu nchini, kaunti ya Kilifi inakodolea hofu ya mkurupuko wa kipindupindu kutokana na utupaji ovyo ovyo wa takataka hasa nepi zilizotumika. Wakizungumza na wanahabari wakati wa zoezi la kufanya usafi wa mazingira mjini Kilifi wadau wa mazingira kaunti hiyo wanawataka wakaazi kutupa takataka katika sehemu maalum zilizotengwa ili kurahisisha ukusanyaji wa takataka hizo na kuepuka kipindupindu katika msimu huu wa mvua ya masika.