- 239 viewsDuration: 1:50Huduma za afya katika Kaunti ya Lamu zimeathiriwa pakubwa kutokana na mgomo wa wauguzi. Wauguzi hao wanadai serikali ya kaunti ya Lamu imeshindwa kutekeleza makubaliano yaliyoafikiwa mwaka jana. Miongoni mwa madai yao makubwa ni malipo ya mishahara ya miezi miwili ya mwaka 2020.