- 171 viewsDuration: 3:45Idadi ya watu waliofariki kwenye mafuriko nchini imeongezeka hadi 85 hii leo, baada ya watoto wawili kufariki kwenye maporomoko ya ardhi katika eneo la Kitende kaunti ya Makueni. Wawili hao walifariki baada ya nyumba yao kufunikwa na matope. Haya yanajiri huku mamia ya watu wakikadiria hasara ya mafuriko katika maeneo mbalimbali.Waziri wa Mazingira Deborah Barasa amewatahadharisha wanaoishi kwenye maeneo hatari kuhamia maeneo salama msimu huu wa mvua.