- 415 viewsDuration: 1:37Idara ya misitu katika kaunti ya Kwale inasema imefikia asilimia 13.9 ya misitu katika kaunti hiyo ikikisistiza idadi hiyo ingali chini. Mhifadhi Mkuu wa Misitu kaunti ya Kwale Elvis Fondo, anasema lengo ni kufikia asilimia 30 ya miti ifikapo mwaka 2032, akisema kuna juhudi zaidi za kukuza miti. Akizungumza katika Shule ya Msingi ya Shimba Hills, afisa huyo amewahimiza wakazi kutumia msimu huu wa mvua kupanda miti mashambani na katika maeneo ya umma, ikiwemo ya matunda kwa manufaa ya wakazi..