Skip to main content
Skip to main content

IEBC: Wapiga kura waliosajiliwa 2012 kwa njia ya kielektroniki hawahitajiki kujisasajili

  • | Citizen TV
    3,743 views
    Duration: 3:18
    Tume huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini IEBC imesema kwamba wapiga kura ambao hawakujisajili kwa njia ya kielektroniki mwaka wa 2012 ndio pekee wanaohitajika kujisalijili na wala sio wote ambao walisajiliwa wakati huo.Hii ni kufuatia tetesi zilizoibuliwa na wananchi ambao walitilia shaka hali yao ya upigaji kura kufuatia taarifa ya mwenyekiti wa Tume hiyo Erastus Ethekon. Na huku baadhi ya wapiga kura wakiibua masuali kuhusu kukosekana kwa vituo vyao vya kupigia kura katika mtandao wa IEBC,Tume hiyo imesistiza kuwa hitilafu hiyo ni ya kimitambo tu.