Skip to main content
Skip to main content

IEBC yafungua mlango kwa wagombea wasio na shahada

  • | BBC Swahili
    12,101 views
    Duration: 2:25
    Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) imefungua mlango kwa wanasiasa wanaotaka kugombea nafasi za kisiasa kama vile Ubunge na Ugavana wanaweza kuruhusiwa kugombea hata kama hawana shahada ya chuo kikuu. Suala hili linatokana na mapigano yanayoendelea ya kisheria kuhusu sharti la wagombea wanaowania nafasi kama vile Mbunge na Gavana kuwa na shahada ya chuo kikuu. Je sifa za kielimu zinapaswa kuamua ustahiki wa uongozi au wapiga kura wanapaswa kuwa na uamuzi wa mwisho. Leila Mohammed ana eleza zaidi. #bbcswahili #kenya #IEBC Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw