Huku tume huru ya uchaguzi na uratibu wa mipaka nchini IEBC ikiendeleza usajili wa wapiga kura wapya, Kaunti ya Bungoma imebainika kusajili idadi ndogo ya wapigaji kura kwenye awamu ya usajili iliyopita.
Akizungumza baada ya mafunzo ya maafisa wa kusimamia usajili wa wapiga kura, meneja wa IEBC kaunti ya Bungoma Grace Rono, amesema kuwa walisajili chini ya asilimia kumi ya idadi waliyotarajia ya zaidi ya elfu kumi na nane. Rono amesema kwa sasa wanalenga vijana zaidi ya elfu sabini na tatu, akiwarai vijana kujitokeza kwa wingi na kusisitiza kuwa kwa wakati huu hakutakuwa na changamoto ya kusafiri mwendo mrefu kusajiliwa.