- 2,158 viewsDuration: 2:56Halmashauri huru ya usimamizi wa utendakazi wa polisi nchini, IPOA, leo imetoa ripoti ya kina ya uchunguzi wa miili iliyopatikana mto Yala zaidi ya miaka kumi iliyopita. Ripoti hiyo ikichora picha ya namna miili 25 ilitolewa kutoka mto huo kati ya mwaka wa 2013 na mwaka jana. Haya yanajiri huku kamati ya wataalamu inayoshughulikia fidia za waathiriwa wa dhulma ikitetea utendakazi wake, kama Brenda Wanga anavyotuarifu.