- 204 viewsShirikisho la kandanda nchini Ivory Coast limetangaza kuwa mashabiki hawatatozwa ada yoyote katika mechi ya leo usiku dhidi ya Emerging Stars ya Kenya. Kenya inaongoza kwa mabao 2-1 baada ya mechi ya mkondo wa kwanza iliyochezwa Nairobi wiki moja iliyopita. Kocha wa Ivory Coast aliwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani nchini humo, na kisha shirikisho likatangaza kiingilio ni bure. Hata hivyo kocha wa Kenya Anthony Kimani anasema vijana wake wamejipanga vilivyo kukabiliana na Ivory Coast ambao wanahitaji ushindi wa bao 1-0 ili kufuzu ilhali Kenya inahitaji sare yoyote.