- 877 viewsDuration: 1:16Jaji Mohamed Abdulahi Warsame ameteuliwa kuziba pengo lililoachwa wazi katika mahakama ya upeo kufuatia kifo cha jaji Ibrahim Mohammed. Tume ya huduma za mahakama - jsc - imeelezea kuridhishwa kwake na utendakazi wa jaji Warsame, ambaye amekuwa akihudumu kama jaji wa mahakama ya rufaa kwa miaka 14. Jaji mkuu Martha Koome alisifia utendakazi wa Warsame na kumtaja kama jaji ambaye maamuzi yake yamekuwa yakiambatana na sheria na kusifia tuzoefu wake kwenye masuala ya sheria. Majaji watano wlaihojiwa na tume ya huduma za mahakama kwa nafasi hiyo. JSC iliteua majaji 15 kujiunga na mahakama ya rufaa mwaka huu na jumla ya majaji 52 katika mahakama tatu kuu mwaka huu.