Skip to main content
Skip to main content

Jamii kaunti ya Wajir imewahimizwa kushiriki zoezi la usajili wa kura

  • | Citizen TV
    279 views
    Duration: 1:29
    Jamii ya Wajir imewahimiza vijana, Wazee na kina Mama kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi linaloendelea la uandikishaji wa wapiga kura nchini. Wito huo ulitolewa wakati wa kongamano la vijana lililolenga kuhamasisha ushiriki wao kupitia kampeni ya “Niko Kadi”, inayolenga kuwachochea vijana, hususan kizazi cha Gen Z, kujiandikisha kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027. Kongamano hilo lilisisitiza umuhimu wa vijana kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kidemokrasia, huku wakihimizwa kufika katika vituo vya uandikishaji na kupata kura zao za mpiga kura.