Jamii ya Waluhya wanaoishi kaunti ya Kilifi wamezindua mpango unaolenga kuweka jamii katika nafasi za kisiasa, kiuchumi na kijamii katika kaunti za pwani.
Kulingana na waandalizi, kuzinduliwa kwa kundi la ‘OBUHAMBANI BWA ABALUHYA kutawawezesha kupigania mamlaka katika serikali ya Kaunti ya Kilifi na kuhakikisha kuwa jamii inajumuishwa na kushauriana katika kufanya maamuzi. Akizungumza wakati wa hafla ya kusherehekea utamaduni wao katika uwanja wa shule ya upili ya Barani mjini Malindi, mwenyekiti wa kikundi hilo Wilson Ahonga alisema kuwa jamii hiyo imetengwa na utawala wa awali wa kaunti licha ya kuchangia pakubwa katika masuala ya maendeleo.