- 49,894 viewsDuration: 1:24Akiwa na umri wa miaka 117, Qamile Marra kutoka Albania huenda ndiye mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani. Anasema siri ya maisha marefu ni kuishi kwa muda ambao Mungu amekupangia. Alizaliwa wakati Albania ikuwa chini ya utawala wa Dola ya Ottoman na alitimiza miaka 36 wiki mbili kabla ya Vita vya Pili vya Dunia kumalizika. Anaishi katika kijiji kimoja nchini Albania kwa karibu maisha yake yote, Marra amekuwa akijilimia chakula chake na kufuga mifugo. Nyumba yake imezungukwa na miti ya matunda. Hata hivyo, umri wake bado haujathibitishwa rasmi. #bbcswahili #Albania #maishamarefu Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw