Skip to main content
Skip to main content

Je, Tanzania kutengwa kidiplomasia?

  • | BBC Swahili
    19,812 views
    Duration: 2:25
    Ndani ya muda mfupi, nchi 16 za Ulaya zilitoa tamko la pamoja zikihimiza kuchukuliwa kwa hatua za haraka, huku Marekani ikitangaza kuwa inatathmini upya uhusiano wake na Tanzania. Umoja wa Mataifa (UN), Jumuiya ya Madola, Umoja wa Afrika (AU) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) pia zimeelekeza macho yao nchini humo kuhusu mwenendo wa uchaguzi na matukio yaliyoufuata. Huu ni mwendelezo wa kile wachambuzi wanakieleza kama "presha ya kawaida ya kimataifa", lakini kwa Tanzania kiwango kilichoonekana safari hii kinaelezwa kuwa kikubwa zaidi kuliko ilivyozoeleka. Kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyotoa jijini Dar es Salaam mbele ya wazee wa jiji imeongeza mjadala huo. Akirejea wakosoaji wa kimataifa, alihoji: "Nje huko wanakaa ooh Tanzania ifanye hivi, ifanye vile… who are you (nyie ni kina nani)? Wanadhani bado ni masters (watawala) wetu?" Mwandishi wa BBC @scolar_kisanga anaiangazia taarifa hii: - - #bbcswahili #Siasa #tanzania #uchaguzi2025 Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw