- 18,266 viewsDuration: 2:39Je, unajua kwamba matatizo ya kifedha yana podumu kwa muda mrefu yanaweza kuathiri afya yako ya akili na mwili? Wasiwasi wa madeni, kodi ya nyumba, ada za watoto na gharama za maisha unaweza kuathiri usingizi, kumbukumbu na uwezo wa kufanya maamuzi. Utafiti uliofanywa nchini Uingereza kwa zaidi ya watu 2,700 unaangazia uhusiano kati ya matatizo ya kifedha ya muda mrefu na kudhoofika kwa uwezo wa kufikiri. Lakini kwa nini hali hii hutokea, na unaweza kufanya nini ili kulinda afya yako unapokabiliwa na changamoto za kifedha? Mwandishi wa BBC Mariam Mjahid na taarifa zaidi Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw