14,929 views
Duration: 45s
Jeshi la Tanzania limekanusha kuhusika na siasa za nchi hiyo na harakati za mitandaoni.
Kaimu mkuregenzi wa habari na uhusiano wa JWTZ , Kanali Bernard Mlunga, amesema kuwa kumekua na baadhi ya watu wanaotumia mtandao kuweka maudhui yanayochochea kuingiza jeshi katika siasa.
Hata hivyo, mapema hii leo, taarifa ya video ilisambaa katika mitandao ya kijamii ikimuonesha mtu mwenye mavazi ya kijeshi ya Tanzania, na kujitambulisha kama afisa wa cheo cha Kapteni akitoa wito wa mabadiliko ya kisiasa na uongozi na kulindwa kwa haki za binadamu nchini humo.
#bbcswahili #tanzania #usalama