Skip to main content
Skip to main content

Jinsi Drone ya Ukraine ilivyomwokoa askari kutoka eneo la mabomu

  • | BBC Swahili
    6,347 views
    Duration: 34s
    Jeshi la Ukraine limetoa video za kile linachodai kuwa ni operesheni ya kwanza duniani ya kumuokoa askari aliyejeruhiwa kutoka mstari wa mbele wa vita kwa kutumia drone. Jeshi hilo lilisema ilikuwa hatari kumfuata askari huyo kwa sababu alikuwa amekwama katika eneo la mabomu na kulikuwa na drone nyingi za Urusi angani. Kwa mujibu wa jeshi hilo, drone kubwa aina ya hexacopter iliyokuwa ikiendeshwa kutoka mbali iliweza kumbeba askari huyo na kumtoa salama katika eneo la hatari, licha ya ugumu wa operesheni hiyo. #bbcswahili #ukraine #drone Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw