Kakan Maiyo kushtakiwa kwa kukosoa serikali atarajiwa kortini Ijumaa

  • | Citizen TV
    2,990 views

    Maafisa wa polisi wanaendelea kumzuilia mfanyabiashara Godfrey Kakan Maiyo katika kituo cha polisi cha Muthaiga baada ya kukamatwa na maafisa wa DCI jijini Nairobi. Hadi sasa, Maiyo aliyekamatwa kwenye duka lake hajafikishwa mahakamani na hajui mashtaka yanayomkabili. Familia yake ikisema haijapewa sababu ya kuzuiliwa kwake na inaitaka serikali kumuachilia huru mara moja