- 1,938 viewsDuration: 3:13Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka ameonya viongozi wa kisiasa dhidi ya kuchochea chuki za kikabila kufuatia mizozo katika mpaka wa Garissa na Kitui. Akizungumza leo katika kituo cha SKM , Kalonzo aliishutumu serikali kwa kulegea kushughulikia shambulizi la Tseikuru na kusema kuwa ni sharti ujangili udhibitiwe kikamilifu ili kuzuia vifo zaidi vya watu wasio na hatia. Wakati huo huo, viongozi kutoka eneo la Kaskazini Mashariki wameshtumu vurugu katika barabara ya Mwingi–Garissa, wakionya kuwa mapigano yanayoendelea yanaweza kuharibu mafanikio yaliyopatikana kwa miaka mingi ya kuishi kwa amani kati ya jamii jirani. Mwanahabari wetu Abdiaziz Hashim na taarifa kamili. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive