- 2,338 viewsDuration: 3:30Kwa miaka mingi, wakulima wamekuwa wakitumia mbegu za maharagwe zilizohifadhiwa kutoka mavuno ya awali, hali ambayo mara nyingi imechangia uzalishaji mdogo, huku upungufu wa madini ya chuma ukiendelea kuwa changamoto ya lishe. Watafiti wa KALRO katika Kaunti ya Trans-Nzoia sasa wanaendesha mpango wa kueneza kibiashara aina ya maharagwe ya Nyota, yenye kiwango cha juu cha madini ya chuma. Mpango huo unalenga kuongeza upatikanaji wa mbegu bora zilizothibitishwa, kuongeza uzalishaji na kuboresha lishe, kama Denis Otieno anavyoangazia kwenye Kilimo Biashara wiki hii.