Skip to main content
Skip to main content

Kamati ya bunge ya uchukuzi yagakua usalama wa uwanja Wilson

  • | Citizen TV
    455 views
    Duration: 2:21
    Kamati ya Seneti kuhusu Barabara, Uchukuzi na Miundombinu imefanya ukaguzi katika Uwanja wa Ndege wa Wilson jijini Nairobi ili kutathmini hali ya uwanja huo katika usimamizi wa majanga. Haya yanajiri kutokana na wasiwasi kuhusu usalama duni katika uwanja huo baada ya ndege kutua kwa kishindo na kuondoka kwenye barabara ya ndege uwanjani humo siku nne zilizopita. Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga wa Kenya (KCA), Emile Nguza Arao, amesema taasisi hiyo ilihusika kikamilifu katika kupendekeza miradi katika uwanjani huo. Hata hivyo, ameeleza kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wa kazi hizo, akisema Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Kenya (KAA) ipo katika nafasi nzuri zaidi kueleza sababu za kuchelewa kwa miradi hiyo.