- 0 viewsKamati ya Bunge kuhusu Fedha imeanza vikao vya umma kukusanya maoni kuhusu Mswada wa Fedha wa mwaka 2026/2027. Kikao cha kwanza kimehusisha makundi na mashirika mbalimbali kutoka sekta ya kibinafsi. Makundi yaliyofika yameeleza wasiwasi wao kuhusu ongezeko la ushuru, hasa kwa wafanyakazi wanaopokea mishahara ya kila mwezi.