Kamati ya maswala ya kigeni imekataa kumuidhinisha Keiru

  • | Citizen TV
    309 views

    Kamati ya bunge ya ulinzi na maswala ya kigeni imekataa kuidhinisha uteuzi wa Charles Githinji Keiru kama balozi wa Kenya katika Jamhuri ya DRC baada ya kukamilisha shughuli ya kuwahoji walioteuliwa na Rais kuwakilisha kenya katika mataifa mbali mbali. Kamati hiyo inayoongozwa na mbunge Nelson Koech iliwaidhinisha wengine wote 25 waliofika mbele yake. Hata hivyo ilikataa kupitisha jina la Keiru kwa kukosa kuwa na taarifa yoyote kuhusu taifa ambalo anapasa kuhudumu. Katika ripoti ya kurasa 89 tume hiyo pia iliwaidhinisha wengine watatu licha ya maswali kuibuka katika kikao cha kuwahoji.