- 2,756 viewsDuration: 2:58Kamati ya uhasibu katika bunge la seneti sasa imeandikia barua idara ya upelelezi ya DCI kuanzisha uchunguzi dhidi ya baadhi ya kaunti na magavana ambao wameshindwa kuelezea matumizi ya fedha kwenye maswali ya mkaguzi wa hesabu za serikali. Aidha kamati hiyo imeitaka tume ya kupambana na ufisadi eacc kuanza uchunguzi mara moja na kuelekeza faili kwa kiongozi mkuu wa mashtaka ya umma.