- 350 viewsDuration: 1:57Kamati inayosimamia utekelezaji wa ripoti ya Kamati ya Kitaifa ya Maridhiano (NADCO) imefika kaunti ya Bungoma kutathmini iwapo mambo muhimu katika ripoti hiyo yanatekelezwa . Naibu gavana wa kaunti ya Bungoma Jenipher Mbatiany ameitaka serikali kuu kukamilisha miradi ambayo imeanzisha kabla ya kuzindua miradi zaidi. Aidha, kamati hiyo imezitaka kaunti zingine kuiga mfano wa ushirikiano mwema uliopo baina ya serikali na bunge la Kaunti ya Bungoma jambo ambalo ni gumu katika kaunti nyingi.