- 421 viewsKampeni za uchaguzi mdogo eneo bunge la magarini zimeshika kasi. Vigogo wa upinzani wakiongozwa na Kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka wanarajiwa kuendelea na kampeni za kumpigia debe mgombea wa chama cha dcp Stanley Kenga. Vyama vya ODM na PAA vimeungana kumpigia debe mgombea wa ODM Harisson Garama Kombe. Spika wa seneti Amason Kingi aliongoza misururu ya kampeni wakiwarai wakazi wa Magarini kumchagua Kombe