- 249 viewsDuration: 10:00Baada ya siku mbili za shughuli za usajili jijini Nairobi, kampuni ya M-ajira sasa imetua jijini Mombasa kuendeleza zoezi la kuwasajili madereva wa malori makubwa kwa nafasi za ajira nchini Saudi Arabia. Maafisa wa M-ajira kwa ushirikiano na SMASCO kutoka Saudi Arabia wataendesha shughuli hiyo kwa siku tatu zijazo katika uwanja wa Tononoka, jijini Mombasa. Zoezi hili linalenga kuwasajili madereva 500 watakaopata fursa za ajira katika taifa hilo la Ghuba.