Watunga sera, wawekezaji na viongozi wa masoko ya fedha wanaangazia namna nchi za Afrika zinavyoweza kutumia rasilimali za ndani za uwekezaji kufadhili miundombinu, nishati, ustahimilivu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na uundaji wa ajira. Wajumbe katika Mkutano wa Tatu wa Masoko Endelevu ya Mitaji jijini Nairobi wanasema kuwa, licha ya wawekezaji wa kitaasisi barani Afrika kusimamia mali zenye thamani ya dola trilioni 4 kupitia mifuko ya pensheni, makampuni ya bima, benki na hazina za utajiri wa taifa, ni takriban asilimia 2.7 pekee ndiyo inayowekezwa katika sekta zenye tija kama vile miundombinu. Haya hapa maelezo ya habari hii na nyingine katika kapu letu la biashara.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive