Katibu wa elimu ya kiufundi na mafunzo Dkt. Esther Muoria ametetea mageuzi yanayoendelea katika sekta ya elimu ya kiufundi TVET, akipuuzilia mbali madai kwamba uzinduzi wa mpango wa ulainishaji wa mfumo wa masomo umeongeza karo na kusababisha mkanganyiko katika taasisi hizo. Akizungumza na wanahabari jijini Nairobi leo, Dkt. Muoria alisema mageuzi hayo yanalenga kuwapa vijana wa humu nchini ujuzi unaowawezesha kuajiriwa katika kipindi kifupi, huku karo ya masomo ikiwa kiwango kisichozidi shilingi elfu 35 kwa kila kitengo cha masomo.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive