Kaunti 14 ziko kwenye hatari ya kukosa mgao wao wa kipindi hiki cha matumizi ya fedha baada ya magavana husika kususia maagizo ya kufika mbele ya kamati ya bunge la seneti na badala yake kuelekea kwa mkutano wa faragha huko Kilifi. Kamati ya Uwekezaji wa Umma ya Kaunti katika bunge la Seneti imeonya kwamba itawasilisha ombi la kuzuiwa kwa ufadhili zaidi kwa kaunti za Lamu, Laikipia, Tharaka Nithi, Muranga, Embu, Baringo, Nandi, Siaya, Tana River, Nyandarua, Mombasa, Makueni, Elgeyo Marakwet na Kajiado baada ya magavana wao kukaidi mialiko ya kufika mbele ya bunge hiyo ili kuangazia jinsi walivyotumia fedha wakati wa mwaka wa fedha wa 2024/2025.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive