Skip to main content
Skip to main content

Kaunti ya Kilifi yafadhili masomo ya wanafunzi 3,500

  • | Citizen TV
    78 views
    Duration: 1:58
    Serikali ya Kaunti ya Kilifi imetoa ufadhili kamili wa masomo kwa zaidi ya wanafunzi 3,500 wa shule za kitaifa chini ya Mpango wa County Scholarship Fund. Haya ni kwa muujibu wa Naibu Gavana Flora Chibule akizungumza wakati wa uzinduzi wa wasifu wa Askofu Thomas Kakala, mjini Malindi. Chibule alibainisha kuwa mpango huo unalenga kushughlikia mahitaji ya dharura kwa wanafunzi wanaohitaji zaidi msaada. Aidha serikali ya kaunti ya Kilifi imepongeza baadhi ya wafadhili eneo hilo wanaowasaidia watoto wasiojiweza kupata elimu.