- 114 viewsDuration: 2:02Serikali ya Kaunti ya Laikipia imethibitisha ushirikiano wake na Chuo Kikuu cha Outspan Global katika hatua inayolenga kuboresha utoaji wa huduma za afya na mafunzo katika kaunti hiyo. Akizungumza baada ya hafla ya kutia saini mkataba wa makubaliano, Gavana wa Laikipia Joshua Irungu amesema wanafunzi watapatiwa nafasi ya mafunzo ya vitendo katika vituo vya afya vya kaunti. Hatua hii inalenga kuboresha ujuzi wao wa utabibu na kuwaandaa vyema kuhudumia jamii.